Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 13:43

Wamarekani wakabiliwa na shinikizo la kiuchumi


Kupanda kwa bei ya mafuta Marekani. Picha na AP
Kupanda kwa bei ya mafuta Marekani. Picha na AP

Watu nchini Marekani wanakabiliwa na shinikizo la kiuchumi lililotokana na ongezeko la bei ya mafuta.

Ongezeko la bei ni kufuatia vikwazo Marekani iliyoviwekea Russia.

Wakati mzozo wa Russia na Ukraine unaendelea na Marekani imeacha ununuzi wa mafuta ya Russia, Wamarekani wanaona ugumu uliopo.

Huko Carlifornia bei ya mafuta ilikuwa tayari juu na kuwalazimisha maafisa wa serikali kutafuta njia ya kutoa msaada.

Chama cha magari Marekani –Tripple A kinaonyesha bei zimepanda kwa zaidi ya senti 40 kwa galoni katika wiki inayomalizika Jumamosi ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.

Imeeleza kuwa bei zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 582 kutoka mwaka mmoja uliopita.

XS
SM
MD
LG