Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 12:24

Marekani yawaonya Wamarekani waliopo Kenya


Eastleigh, Nairobi, Kenya
Eastleigh, Nairobi, Kenya

Serikali ya Marekani imewaonya raia wake dhidi ya kutembelea maeneo fulani nchini Kenya.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje jana Alhamisi ilitoa ilani kwa Wamarekani wanaotembea nchini Kenya kutoyatembelea maeneo ya Lamu katika pwani ya nchi hiyo, na mtaa wa Eastleigh, ulio mjini Nairobi.

Afisa wa polisi, barabarani Eastleigh, mjini Nairobi
Afisa wa polisi, barabarani Eastleigh, mjini Nairobi

Gazeti la 'Daily Nation' limenukuu taarifa ya wizara hiyo ikisema kuwa idara ya safari za ndege ya Marekani (FAA) imetuma taarifa kwa mamlaka ya safari za ndege nchini Kenya na kuelezea hofu ya uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi ambayo huenda yakalenga Wamarekani na raia wengine wa mataifa ya magharibi.

Taarifa hiyo ya FAA haikutoa habari kuhusu sehemu ambazo zingelengwa na magaidi, lakini ikaonya kuwa huenda magaidi hao wakajaribu kutumia vifaa vinavyobebwa na watu na ambavyo vina uwezo wa kutungua ndege wakati inapopaa.

XS
SM
MD
LG