Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:05

Wamalawi wapiga kura kumchagua rais mpya


Upigaji kura ukiendelea katika wilaya ya Machinga iliyopo kaskazini mwa Blantyre nchini Malawi
Upigaji kura ukiendelea katika wilaya ya Machinga iliyopo kaskazini mwa Blantyre nchini Malawi
Wananchi wa Malawi wanapiga kura Jumanne kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa pamoja wa kuchagua vyombo vitatu vya serikali, rais mpya, bunge na serikali za mitaa.

Rais Joyce Banda aliyechukua madaraka mwaka 2012 baada ya kufariki kwa aliyemtangulia Bingu wa Mutharika, akiwa anapendwa sana na wananchi lakini hii leo anakabiliana na upinzani mkali kutoka wagombea wengine 11 wanaowania kiti cha rais kutokana na kashfa ya fedha iliyopewa jina la ‘cashgate’.

Wapinzani wake wakuu ni pamoja na kaka wa bwana Mutharika, Peter, mchungaji wa zamani Lazarus Chakwere na Atupele Muluzi ambaye ni mtoto wa kiume wa Rais wa zamani Bakili Muluzi.

Katika kampeni zao wagombea kiti cha rais walizungumzia masuala ya kiuchumi katika kampeni zao ili kuweza kuinyenyua nchi kusonga mbele.

Upigaji kura ulichelewa kwa saa kadhaa Jumanne katika baadhi ya wilaya ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa kibiashara Blantyre.

Zaidi ya watu milioni saba wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali.
XS
SM
MD
LG