Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 29, 2020 Local time: 05:21

Kadinali Wamala aruhusiwa kutoka hospitali nchini Uganda


kadinali Emmanuel Wamala

Kadinali Emmanuel Wamala ametoka Hospitali ya Nsambya ambapo alikuwa amelazwa kutokana na matatizo ya afya tangia Jumapili.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uganda Kardinali huyo ambaye ana umri wa miaka 90 aliruhusiwa kuondoka hospitali Jumanne majira ya saa kumi jioni baada ya kile kilichoelezwa na vyanzo hivyo kwamba “alikuwa akifanyiwa mtibabu ya kina na wataalamu mbalimbali.”

Kabla ya hapo alikuwa amegunduliwa kuwa na tatizo la pneumonia lakini vyanzo vingine karibu na Kadinali huyo vimeeleza kuwa alikuwa na uchovu.

“Naweza kukuthibitishia tayari ameruhusiwa kutoka hospitali na ametakiwa kupumzika. Amepata nafuu kubwa,” chanzo karibu na Kadinali kimesema Jumatatu.

Amepelekwa kwenye nyumba ya Kadinali ya Nsambya ambako ataendelea kupumzishwa na kusimamiwa na Padri Paul Mugerwa. Kadinali Wamala ni mkazi wa nyumba hiyo.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG