Mawakili wa rais huyo, ambaye alipinduliwa Julai 26 na kuwekwa kizuizini tangu wakati huo, pia wamesema katika taarifa yao kuwa wanakata rufaa kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.
Malalamiko hayo, ambayo shirika la habari la AFP iliyaona siku ya Jumatatu, yanamlenga jenerali mpya Abdourahamane Tiani na "wengineo".
Inajumuisha madai ya kiraia "mashambulizi na njama dhidi ya mamlaka ya serikali, uhalifu na makosa yaliyofanywa na watumishi wa umma na ukamataji kiholela na kutiwa ndani.
Mashitaka hayo yanatarajiwa kuwasilishwa siku chache zijazo katika mahakama iliyoko katika mji mkuu Niamey, mmoja wa mawakili, Dominique Inchauspe, aliliambia shirika la habari la AFP.
Mawakili hao pia walisema wanakata rufaa kwa vyombo viwili vya Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kundi lake linaloshughulikia kuwekwa vizuizini kiholela.
Wakati huo huo, viongozi wa mapinduzi wamekubali upatanishi wa Algeria na "mpango wa mpito wa miezi sita" ili kurejesha "utaratibu wa kikatiba" katika nchi hiyo ya jirani ya kiafrika, Wizara ya mambo ya nje ya Algeria ilitangaza Jumatatu.
"Serikali ya Algeria imepokea kupitia wizara ya mambo ya nje ya Niger (taarifa ya) kukubali upatanishi wa Algeria unaolenga kuunga mkono suluhu ya mgogoro wa kisiasa wa Niger," Algiers ilisema katika taarifa yake.
Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP
Forum