Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 10:14

Walinzi wa amani Somalia kufikia 8,000


Viongozi wa Umoja wa Afrika wameidhinisha kupeleka wanajeshi elfu mbili zaidi Somalia na kufanya idadi ya walinzi wa amani huko kufikia 8,000.

Viongozi wa Umoja wa Afrika wamekubaliana kupeleka wanajeshi 2,000 zaidi huko Somalia kuongezea nguvu jeshi la ulinzi wa amani la AU ambalo sasa litakuwa na jumla ya karibu wanajeshi 8,000.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati mkutano wa viongozi hao unaelekea siku ya mwisho leo. Jeshi la sasa la AU huko Somalia lina wanajeshi kutoka Uganda na Burundi pekee lakini mwenyekiti wa tume ya AU, Jean Ping, anasema Guinea iko tayari kupeleka wanajeshi hao wa nyongeza.

Waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani Johnnie Carson alikutana na viongozi kadha wa Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki Jumatatu. Alisema viongozi hao wameonyesha nia ya kuongeza jeshi la ulinzi kupambana na al-Shabab - kundi la wanamgambo wenye sera kali za kidini linalojaribu kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia.

XS
SM
MD
LG