Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 06:51

Walinda amani wanane wa Umoja wa mataifa wafariki katika ajali ya ndege mashariki mwa DRC.


 Wanajeshi wa tume ya Umoja wa mataifa nchini DRC (MONUSCO) wakifanya doria katika wilaya ya Djugu, mkoa wa Ituri, mashariki mwa DRC, Machi 13, 2020. Picha ya AFP.
Wanajeshi wa tume ya Umoja wa mataifa nchini DRC (MONUSCO) wakifanya doria katika wilaya ya Djugu, mkoa wa Ituri, mashariki mwa DRC, Machi 13, 2020. Picha ya AFP.

Msemaji wa Umoja wa mataifa amesema Jumanne kwamba hakuna aliyenusurika wakati helikopta ya tume ya Umoja wa mataifa nchini DRC (MONUSCO) ilipofanya ajali mashariki mwa nchi hiyo ikiwa na walinda amani wanane wa Umoja wa mataifa.

Mapema, msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric alisema helikopta hiyo ilikuwa imebeba watu sita, wote wakiwa wanajeshi wa Pakistan, pamoja na maafisa wawili wa jeshi, mmoja kutoka Serbia na mwingine kutoka Russia, ilipoanguka katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Dujarric alisema kundi hilo la wanajeshi lilikuwa kwenye shughuli ya upelelezi katika eneo la Tshanzu, kusini mashiriki mwa mji wa Rutshuru.

Alisema “ Helikopta ilikuwa imekwenda huko kufuatilia hali eneo ambapo kulikuwa kunafanyika mapigano.”

Amejizuia kueleza kilichosababisha ajali hiyo, akisema uchunguzi unafanyika.

Katika tukio jingine, jeshi la DRC liliwashtumu waasi wa kundi la M23 kudungua helikopta hiyo na kusema kwamba ilidunguliwa katika eneo linalodhibitiwa na waasi hao.

Katika mahojiano na idhaa ya kifaransa ya Sauti ya Amerika, msemaji wa M23 Willy Ngoma, naye amelishtumu jeshi la DRC kudungua ndege hiyo wakati likiwafyatulia risasi wapiganaji wa M23.

XS
SM
MD
LG