Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:19

Walinda amani wa UN wauwawa Mali


Wanajeshi wa Mali washika doria karibu na mpaka wa Niger. Agosti 23, 2021
Wanajeshi wa Mali washika doria karibu na mpaka wa Niger. Agosti 23, 2021

Umoja wa Mataifa umesema kwamba walinda amani wake watatu wameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya Jumatatu baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa barabarani kaskazini mwa Mali.

Wanamgambo wanaohusishwa na kundi la kigaidi la al Qaida wamekuwa wakifanya mashambulizi nchini humo kwa miaka kadhaa sasa. Msemji wa Umoja huo Stephane Dujarric amesema kwamba walinda amani hao walikuwa wakiondoa vilipuzi vya kutegwa ardhini kwenye makazi ya kaskazini ya Tassalit kwenye jimbo la Kidal wakati wa tukio hilo. Waliyo jeruhiwa wanaendelea kupata hospitalini ripoti imeongeza. Mwaka huu pekee, walinda usalama 12 wa Umoja wa Mataifa wmeuwawa nchini humo, shambulizi la Jumatatu likiwa la karibu zaidi.

XS
SM
MD
LG