Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 06:25

Walibya waadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi


Wananchi wakiwa na bendera za ufalme wa Libya wamekusanyika wakati wa sherehe za mapinduzi ya Februari 17 huko Benghazi.

Walibya wafanya sherehe mbali mbali nchini humo kuadhimisha mwaka mmoja wa Mapinduzi tangu kuangushwa Moammar Gadhafi.

Wananchi wa Libya wanasheherekea mwaka mmoja wa mapinduzi ambayo yalioangusha utawala wa dikteta wa zamani Moammar Gadhafi.

Sherehe mbali mbali zilianza katika miji kote nchini humo.

Katika mji wa mashariki wa Benghazi maafisa wa usalama walikuwa kwenye tahadhari kubwa wakati mamia ya watu wakishangilia huku wakipeperusha bendera nje ya mahakama ya mji huo. Sherehe rasmi zinatarajiwa mjini humo Ijumaa.

Walibya wengi walielezea kuridhishwa na kuwa na matumaini mazuri na mafanikio yaliopatikana tangu mapinduzi hayo.

Hata hivyo waziri wa zamani wa serikali Ali Al Tahrouni alisema bado kuna kazi ya kufanya.

XS
SM
MD
LG