Siku ya Jumapili, ECOWAS iliiwekea vikwazo Niger na kuonya kuwa inaweza kutumia nguvu huku ikiupa utawala wa kijeshi muda wa wiki moja kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum.
Afisa wa ECOWAS pia aliiambia AFP jana Jumanne kwamba ujumbe wa jumuiya hiyo unaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar utafanya ziara Niger leo Jumatano.
Mapinduzi hayo yamezitia wasiwasi nchi za magharibi zinazojitahidi kudhibiti uasi wa wanamgambo wa kiislamu uliozuka kaskazini mwa Mali mwaka 2012, na kuingia Niger na Burkina Faso miaka mitatu baadaye na sasa unatishia mataifa dhaifu katika Ghuba ya Guinea.
Raia kadhaa, wanajeshi na polisi wameuawa katika eneo hilo lote, wengi katika mauaji ya kikatili, huku watu milioni 2.2 nchini Burkina Faso pekee wakiwa wamehama makazi yao.
Forum