Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 04:05

Wakuu wa kijeshi wa ECOWAS kukutana wiki hii nchini Ghana


Maafisa waandamizi wa jeshi la Senegal
Maafisa waandamizi wa jeshi la Senegal

Wakuu wa kijeshi kutoka jumuiya ya Afrika Magharibi, ECOWAS watakutana nchini Ghana wiki hii, kujadili uwezekano wa kuingilia kati mzozo wa Niger, vyanzo vya kijeshi na kisiasa katika kanda hiyo vilisema Jumanne.

Mkutano wa Alhamisi na Ijumaa -- uliopangwa kufanyika wikendi iliyopita lakini ukaahirishwa -- unakuja baada ya viongozi wa ECOWAS, wiki iliyopita kuidhinisha kutumwa kwa "kikosi cha kusubiri kurejesha utulivu wa kikatiba" nchini Niger, ambayo rais wake alipinduliwa Julai 26.

Mkutano wao wa kilele uliofanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja Alhamisi iliyopita, pia ulitsisitiza azma ya jumuiya hiyo, ya kutafuta suluhu la kidiplomasia kwa mzozo huo.

Uchaguzi wa Rais Mohamed Bazoum mwaka 2021 ulikuwa wa kihistoria katika historia ya Niger, ukipelekea makabidhiano ya amani ya kwanza ya nchi hiyo tangu uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960.

Kuondolewa kwake kulizua wimbi la mshtuko kote Afrika Magharibi, ambapo Mali na Burkina Faso – ambazo pia zianakabiliana na wanamgambo wa Kiislamu-- pia zimeshuhudia mapinduzi ya kijeshi.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) iliwapa watawala wa kijeshi wa Niger makataa ya wiki moja, hadi Julai 30 kurejesha Bazoum au kukabiliana na uwezekano wa matumizi ya nguvu, lakini muda wa mwisho ulimalizika bila hatua yoyote kuchukuliwa.

Wachambuzi wanasema uingiliaji kati wa kijeshi ungekuwa hatari kiutendaji na pia kisiasa, ikizingatiwa mgawanyiko ndani ya ECOWAS na ukosoaji wa ndani.

Forum

XS
SM
MD
LG