Wakulima kote Ulaya kwa wiki kadhaa sasa wamekuwa wakiandamana kupinga kile wanachosema ni kanuni kandamizi za kimazingira, ushindani kutokana na bidhaa za gharama ya chini kutoka nje ya EU, pamoja na mapato ya chini.
Barabara iliofungwa na wakulima hao ni ile ya A2 karibu na mji wa Slubice, ulioko mashariki mwa Poland, karibu na mpaka wa Ujerumani. Mwanzoni, walipanga kufunga barabara hiyo kwa siku 25, lakini walipunguza muda huo baada ya mashauriano na wawakilishi wa utawala wa kieneo, wafanyabiashara pamoja na wasafirishaji bidhaa.
Mmoja wa viongozi wa wakulima hao Dariusz Wrobel, alisema kwamba wamekubali kufungua barabara hiyo ifikapo Jumatatu. Hata hivyo, hilo litategemea masuala yasioweza kutabirika, ameambia shirika la habari la AFP. Mawaziri wa Kilimo kutoka mataifa wanachama wa EU, wamepangiwa kukutana Jumatatu mjini Brussels.
Forum