Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 22:59

Wakufunzi zaidi wa jeshi la Russia wawasili nchini Niger


Picha hii inaonyesha inaonyesha wanajeshi wa Russia wakipakua vifaa kwenye ndege ya kijeshi ya mizigo kwenye kambi ya jeshi la anga mjini Niamey, Aprili 10, 2024. Picha ya AP
Picha hii inaonyesha inaonyesha wanajeshi wa Russia wakipakua vifaa kwenye ndege ya kijeshi ya mizigo kwenye kambi ya jeshi la anga mjini Niamey, Aprili 10, 2024. Picha ya AP

Wakufunzi wapya wa jeshi la Russia na vifaa vya kijeshi viliwasili nchini Niger, kulingana na televisheni ya serikali katika taifa hilo la Afrika ambalo linataka wanajeshi wa Marekani waondoke nchini humo.

Kundi la kwanza la wakufunzi 100 wa Russia waliwasili nchini Niger tarehe 10 Aprili pamoja na mifumo ya ulinzi wa anga.

Ndege mbili za mizigo za kijeshi ziliwasili Jumamosi, kulingana na televisheni ya Tele Sahel na kwamba Russia kwa sasa imepeleka ndege tatu za mizigo na vifaa vya kijeshi na wakufunzi mwezi uliopita.

The Africa Corps, linalochukuliwa kama mrithi wa kundi la Mamluki wa Russia la Wagner barani Afrika, limethibitisha kuwasili kwa wakufunzi katika taarifa kwenye mtandao wake wa Telegram.

Jumamosi, kundi hilo lilisema wakufunzi zaidi, vifaa, na bidhaa za chakula ziliwasili.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Llyod Austin alieleza Alhamisi kwamba wanajeshi wa Russia sasa wapo katika kambi ya jeshi la anga karibu na uwanja wa ndege wa Niamey, kambi ambayo pia inatumiwa na wanajeshi wa Marekani.

Utawala wa kijeshi, ambao ulichukua madaraka mwezi Julai 2023 katika mapinduzi, uliwafukuza wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa nchini humo na kisha kukosoa makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Marekani.

Ulisema makubaliano hayo “yalilazimishwa na upande mmoja” na Washington. Washington ilikubali mwezi Aprili kuondoa wanajeshi wake 1,000 nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG