Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 09:27

Wakongwe wawili wa kisiasa wanawania kuwa rais ajaye wa Nigeria


Mgombea urais wa Nigeria Atiku Abubakar, wa chama cha People's Democratic Party (PDP). Alipohudhuria mkutano wa kampeni za uchaguzi kwenye Uwanja wa Tafawa Balewa, mjini Lagos, Nigeria, Februari 12, 2019.(Picha AP /Sunday Alamba).

Wakongwe wawili wa kisiasa wenye umri wa miaka ya 70 wanawania kuwa rais ajaye wa Nigeria, na kuahidi sera zinazounga mkono biashara na kufufua uchumi mkubwa zaidi barani Afrika kwa kurekebisha sekta yake ya mafuta na kuzuia vitisho vya usalama vilivyoenea.

Chama tawala cha All Progressives Congress (APC) wiki hii kilimchagua Bola Tinubu kuwa mgombea wake kuchukua nafasi ya Rais Muhammadu Buhari katika kura ya mwaka ujao. Atakabiliana na Atiku Abubakar, makamu wa rais wa zamani na mwanasiasa mkongwe ambaye ni mpeperushaji bendera wa chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP).

Abubakar hapo awali aligombea kwa ahadi ya kubinafsisha shirika la taifa la mafuta linalomilikiwa na serikali na kuanzisha hazina ya kuchochea uwekezaji wa miundombinu ya kibinafsi. Kwa upande wake, Tinubu anaahidi kuongeza viwanda ili kupunguza utegemezi wa Nigeria wa kuagiza bidhaa kutoka nje, kujenga bandari ya bahari ya kina kusini na kuongeza utafutaji wa gesi na mafuta katika nchi hiyo mzalishaji mkuu wa mafuta ghafi barani Afrika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG