Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:26

Wakimbizi wa cameroon hatarini ya kukabiliwa na njaa


Wakimbizi wa Cameroon.
Wakimbizi wa Cameroon.

Naibu Mkurugenzi wa idara ya dharura ya Umoja wa Mataifa, Ursula Mueller alisema kwamba maelfu ya watu wanaotafuta hifadhi huko Cameroon baada ya kukimbia ghasia nchini mwao watakabiliwa na njaa ikiwa msaada wa fedha hautapatikana.

Mueller alisema wafadhili hadi hivi sasa wametoa asilimia tano ya dola milioni 305 zinazohitajika kwa Cameroon mwaka huu. Matatizo ya wakimbizi huko Cameroon yanaongezeka kutokana na mapigano katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya kati-CAR.

Wakati huo huo maelfu ya wa-Nigeria wamekimbia kuingia Cameroon kuepuka mashambulizi yanayofanywa na kundi la wanamgambo wa ki-Islam la Boko Haram ambalo lilianza uasi mwaka 2009 katika juhudi za kuunda taifa la ki-Islam. Kundi la Boko Haram pia limeshambulia huko kaskazini mwa Cameroon na kupelekea ghasia mbaya.

Hivi sasa watu milioni 3.3 wanahitaji msaada ongezeko la takribani asilimia 15 ikilinganishwa na mwaka 2017, Umoja wa Mataifa ulisema.

XS
SM
MD
LG