Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:09

Wakimbizi wa Sudan Kusini Wasababisha Mzozo Barani Afrika


Kambi ya wakimbizi Sudan Kusini
Kambi ya wakimbizi Sudan Kusini

Tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe Desemba 2013 nchini Sudan Kusini, idara hiyo ya Umoja wa Mataifa imeripoti kuwa zaidi ya watu milioni 3.5 wamelazimika kukimbia makazi yao.

Zaidi ya watu milioni mbili wamekoseshwa makazi ndani ya nchi na zaidi ya milioni 1.5, wamechukua hifadhi katika nchi sita nazo ni Uganda, Ethiopia, Sudan, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

UNHCR inaripoti ongezeko kubwa la idadi ya watu waliokimbia Sudan Kusini mwaka jana, huku zaidi ya watu 760,000 wakiomba hifadhi.

Msemaji wa idara hiyo, William Spindler anasema msafara ulisambaa kufuatia mapigano makali katika mji mkuu Juba, baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya amani kati ya serikali na majeshi ya waasi.

“Kwa wastani watu 63,000 walilazimika kuondoka nchini kila mwezi. Takriban nusu milioni walikimbia katika kipindi cha miezi minne tangu Septemba 2016 …. Wengi wakiwasili wakiwa na viwango vikubwa vya utapiamlo -- wakiwa na athari mbaya kutokana na ukatili kwa sababu ya vita vinavyoendelea,” amesema Spindler.

Msemaji huyo amesema wakimbizi wapya wanaowasili wameripoti kuhusu kusambaa kwa majanga ndani ya Sudan Kusini, ikiwemo mauaji, utekaji nyara, ubakaji na uhaba mkubwa wa chakula. Wakimbizi wanasema wamelazimika kukimbia wakikhofia maisha yao.

Amesema hakuna suluhisho linalojitokeza kwa mzozo huo ambao unaingia mwaka wanne. huku idadi ya wakimbizi ikiongezeka, akisema na mahitaji nayo yakiongezeka hali kadhalika. Anasema idara yake ina uhaba mkubwa sana wa fedha tasimu na hili ni suala ambalo linatia wasi wasi mkubwa.

Anasema UNHCR inahitaji dola milioni 782 kufanya operesheni za kibinadamu ndani ya sudan na katika nchi sita ambao ni wenyeji wa wakimbizi hao.

XS
SM
MD
LG