Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:54

Wakenya waunga mkono katiba mpya


Kufuatana na matokeo ya awali, wa Kenya wengi wanaonekana wameunga mkono katiba mpya inayotazamiwa kuleta mabadiliko makubwa katika nchi hiyo.

Matokeo ya awali kutokana na kura ya maoni nchini Kenya yanaonyesha kwamba wapiga kura kwa wingi mkubwa wameunga mkono mapendekezo ya katiba mpya.

Matokeo hayo ya awali yanaonyesha kwamba theluthi mbili za kura zilizokwisha hesabiwa zinaunga mkono hati hiyo mpya iliyoungwa mkono kwa nguvu na Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga.

Kufuatana na matokeo kutoka kwa tume ya mpito ya uchaguzi huko Kenya kura ya ndiyo imeweza kujipatia asilimia 67 za kura na kura ya hapana imejipatia asili mia 33 hadi Jumatano usiku. Lakini matokeo rasmi yanatarajiwa Alhamisi jioni. Ili rasimu hiyo kuweza kuidhinishwa na kuwa sheria kunahitajika zaidi ya asili mia 50 za kura ya ndiyo.

XS
SM
MD
LG