Kipchoge, ambaye ni raia wa Kenya, alishinda mbio hizo kwa kukimbia kwa muda wa saa mbili, dakika tatu na sekunde 32.
Hata hivyo, hakuweza kufikia kiwango cha ubingwa wa kimataifa kwa sekunde 35 kutokana na hali ya unyevu uliosababishwa na mvua.
Mwanariadha huyo alinukuliwa na shirika la habari la Associated Press, AP, akisema kuwa mbio hizo zilikuwa ngumu kuliko mbio zingine zote za Marathon ambazo amewahi kushiriki.
Adola alimaliza mbio hizo sekunde 14 nyuma ya Kipchoge. Kwa upande wa wanawake, Mkenya Gladys Cherono alishinda mbio hizo kwa kukimbia kwa muda was aa mbili, dakika 20 na sekunde 23.