Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 20:00

Wakenya wapinga ongezeko la mishahara kwa wabunge


Maandamano dhidi ya wabunge wa Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Polisi wa kupambana na ghasia nchini Kenya walifyatua gesi ya kutoa machozi na mabomba ya maji Jumanne ili kusambaratisha kiasi cha waandamanaji 200 waliokusanyika nje ya bunge wakiandamana dhidi ya madai ya mishahara ya wabunge.

Wakati huo huo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alizungumzia suala hili na kusema kuwa wabunge wanastahili kusahau nyongeza hii ya mishahara. “saa nyingine unasikia uchungu badala ya kuwa sasa tunajiuliza how are we going to serve our people we are asking ourselves how are we going to get more money in our pockets tafadhalini kwanza tufanye yale ambayo ni muhimu na hiyo ni kutumikia wananchi wetu”.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:13 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Makundi ya haki za kiraia yaliandaa maandamano yaliopata uungaji mkono kupitia mitandao ya kijamii ili kuelezea hasira za wakenya ambapo wanasiasa wanadai mapema nyongeza ya mishahara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika kwa amani hapo Machi 4.

Watayarishaji wa maandamano ya “kulidhibiti bunge” walisema lengo lao ni kusaidia kuwafichua wanasiasa wenye tamaa na walaji rushwa katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa Afrika mashariki.

Waandamanaji waliwanywesha nguruwe damu kwenye milango ya bunge katika mji mkuu Nairobi kama ishara kwa wabunge kuonesha ishara ya “tamaa.”

“Tumesambaza damu ya nguruwe kuonesha kwamba wabunge wana tamaa kama nguruwe” alisema Boniface mwangi kabla ya yeye na waandaaji wengine kukamatwa na polisi.
XS
SM
MD
LG