Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:36

Wakenya walioshtakiwa ICC kufanya mkutano wa hadhara Nairobi .


Mstari wa mwisho ni waziri wa zamani wa elimu wa Kenya William Ruto , kushoto waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgey na mtangazaji Joshua Sang, kulia, wakiskiliza mashtaka dhidi yao huko The Hague Uholanzi, Aprili 7, 2011
Mstari wa mwisho ni waziri wa zamani wa elimu wa Kenya William Ruto , kushoto waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgey na mtangazaji Joshua Sang, kulia, wakiskiliza mashtaka dhidi yao huko The Hague Uholanzi, Aprili 7, 2011

Wanasiasa wanaokabiliwa na kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya wanatarajiwa kufanya mkutano ambao matamshi yake yanaweza kuwaingiza matatani.

Wanasiasa ambao wako karibu na washukiwa wa ghasia za kikabila za mwaka 2008 huko Kenya wanatarajiwa kufanya mkutano mkubwa Jumatatu mjini Nairobi. Mkutano huo utafanyika licha ya kwamba mmoja wa majaji watatu wa mahakama ya uhalifu wa kimatiafa ya The Hague huko Uholanzi, kutoa onyo kali kwa washukiwa hao waliofikishwa mbele yake, kuwa ikiwa watafanya mikutano na watoe matamshi yanayoweza kuleta hali ya wasiwasi, basi hati ya kukamatwa kwao itatolewa, na watalazimika kupelekwa The Hague ambako watazuiliwa wakisubiri kufanyiwa kesi.

Wakati jaji huyo ametoa matamshi hayo, waziri wa Mambo ya ndani wa Kenya Profesa George Saitoti, aliwasihi wanasiasa hao wajizuie kadiri wawezavyo kutotoa matamshi yanayoweza kuleta wasiwasi.

“Wakati huu ni wakati mugumu sana. Kutokana na hali hiyo, sisi sote lazima tujaribu tuwezavyo kuhakikisha kwamba tunakabili vilivyo hali ya matamshi machungu. Ni kweli watu wana uhuru wa kujieleza lakini lazima tufanya kile tunachotarajia kufanya tukifungamana na sheria” alisema Profesa George Saitoti.

Katika habari nyingine, inasemekana kwamba huenda wanasiasa wengine ambao wako karibu sana na waziri mkuu Raila Odinga, watafanya mkutano Jumatatu kueleza na kusisitiza umuhimu wa amani kwa wakati huu ambapo washukiwa hao sita wanasubiri kufanyika kwa kesi yao mwezi Septemba mwaka huu.

Wakati huo huo kuna habari za kuaminika kwamba mwezi wa sita mwaka huu, huenda kundi la William Ruto na Uhuru Kenyatta likaanzisha chama chake kipya cha kisiasa na kuhama kile cha Orange Democratic Movement (ODM) ambacho kinara wake ni Raila Odinga.

Kuanzishwa kwa chama hicho kunakuja wakati ambapo joto la kisiasa limepamba moto hapa Kenya. Kwa sasa wanasiasa wameanza kujitayarisha kwa uchaguzi wa Ubunge na Urais wa mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG