Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 03:42

Waandamanaji wamtaka waziri wa mambo ya ndani Kenya kufutwa kazi


Wanajarakati wa Kenya waliingia mitaani Jumanne wakitaka serikali kumfukuza kazi mkuu wa polisi na waziri wa mambo ya ndani kwa kushindwa kulinda umma.

Maandamano yamefanyika siku chache baada ya wanamgambo wa kikundi cha Kisomali cha Al Shabab kushambulia basi kaskazini mwa nchi hiyo na kuua watu 28.

Waandamanaji wanasema wamechoshwa kuomboleza watu wasio na hatia.

Waandamanaji walijikusanya nje ya ofisi ya rais karibu siku nzima, na kubeba mamia ya misalaba iliyopakwa rangi nyekundu, ikiashiria wale wote waliouliwa katika mashambulio ya kigaidi na matukio ya uhalifu nchi nzima.

Mmoja wa wanaharakati na waandaaji wa maandamano Boniface Mwangi, ameiambia Sauti ya Amerika, kwamba rais lazima awafute kazi Waziri wa mambo ya ndani Joseph Ole Lenku na mkuu wa polisi David Kimaiyo.

Tunamtaka rais kuitisha uchunguzi kuhusu matukio yote ya ugaidi na kwa nini idara za usalama zimeshindwa kufanya kazi. Kama hawezi kumfukuza kazi Ole Lenku ama Kimaiyo anapaswa kuwaomba wajiuzulu. Alisema Boniface Mwangi.

Kenya imeshuhudia mfululizo wa mahambulizi hatari kwa miaka mitatu iliyopita tangu ilipopeleka vikosi vyake Somalia kupigana na Al Shabab. Shambulizi kubwa lilikuwa katika jengo la maduka ya kifahari ya Nairobi mwezi Septemba 2013 na kuua zaidi ya watu 70.

XS
SM
MD
LG