Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:48

Wakazi wakimbia makazi yao Mashariki mwa DRC kuhofia waasi wa M23


Children fleeing fighting in Rwanguba DRC.
Children fleeing fighting in Rwanguba DRC.

Wasiwasi mkubwa umeshuhudiwa katika Mji wa Rutshururu huko Kivu Kaskazini Mashariki mwa Congo kufuatia uwepo wa waasi wa M23 katika eneo jirani na Matebe .

Wasiwasi mkubwa umeshuhudiwa katika Mji wa Rutshuru huko Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC kufuatia uwepo wa waasi wa M23 katika eneo la karibu na Matebe .

Mkaazi wa Rangira eneo lililopo kilometa chache mashariki mwa Mji wa Rutshuru aliyehifadhi jina lake ameshuhudia mapigano makali kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo FARDC.

Katika eneo la Rangira karibu na kijiji cha Matebe ambako waasi wa M23 wameonekana na kuwatia khofu watu na hvyo kukimbia makazi yao.

Wakazi wengine wameliomba jeshi la serikali kuwajibika vilivyo ili warudi kwa mara nyingine kwenye vijiji vyao.

Waasi wamefika katika eneo hilo huku bado jeshi likiwa mbali kabisa kwenye mstari wa mbele wa mapigano eneo la Rwanguba na Busanza.Wakazi hao waliondoka eneo la Matebe kwa hofu ya kujeruhiwa wakati wa mapigano makali.

Msemaji wa jeshi la Congo Cilvin Ekenge alisema taifa hilo lipo hatarini kuvamiwa na waasi wanaosaidiwa na mataifa jirani ya Congo katika eneo la Afrika Mashariki na lazima vyombo vya habari pamoja na wakaazi kulinda usalama wa taifa wakishirikiana na serikali kuepuka kutangaza habari mbaya kuhusu jeshi.

Jeshi bado linaendelea kukabiliana na waasi wa M23 wanaoomba mazungumzo na serikali huku serikali ikisema ni kundi la kigaidi ambalo linayumbisha usalama wa DRC kwa kusaidiwa na mataifa jirani na serikali kuzungumza nao.

Imeandaliwa na Austere Malivika VOA Mashariki mwa DRC.

XS
SM
MD
LG