Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:08

Wakazi wa Kinshasa wakimbia wakihofia kuzuka ghasia

Wanachama wa upinzani UDPS wakishikilia picha za Etienne Tshisekedi zilizo na damu baada ya walinzi wa rais kufyatua risasi kwenye kundi la watu nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa,NDjili huko Kinshasa.

Maelfu ya watu wanaoripotiwa kufikia 3000 wamekimbia jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakihofia mlipuko wa ghasia.

Maelfu ya watu wanakimbia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakihofia kwamba matokeo ya uchaguzi yatakayotangazwa jumanne yanaweza kupelekea kulipuka ghasia .

Polisi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Congo wanasema watu wapatao 3,000 wamewasili katika mji mkuu Brazaville tangu Desemba 2.

Maafisa wanasema wengi wa waliowasili wanatoka mji mkuu wa DRC Kinshasa ambao wanaishi kwenye eneo la mto Congo kutoka Brazaville ambapo hali ni ya mvutano.

XS
SM
MD
LG