Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 00:00

400 wakamatwa Russia, kwa kutoa heshima kwa Navalny


Zaidi ya watu 400 wameshikiliwa nchini Russia, wakati wakitoa heshima kwa kiongozi wa upinzani Alexey Navalny, ambaye amefariki dunia katika eneo la mbali la Arctic, shirika maarufu la kutetea haki za binadamu limeripoti.

Kifo cha ghafla cha Navalny, 47, kimekuwa pigo kubwa kwa raia wengi wa Russia, ambao walikuwa na matumaini ya siku zijazo akiwa ni mkosoaji mkubwa wa Rais Vladimir Putin.

Navalny alibaki kama sauti pekee kwa ukosoaji wake usio na kikomo wa Kremlin hata baada ya kunusurika na sumu ya neva na kupokea vifungo vingi gerezani.

Habari hizo zimeenea ulimwenguni kote, na mamia ya watu katika miji kadhaa ya Russia, walimkumbuka kwa kuweka mashada ya maua na kuwasha mishumaa Ijumaa na Jumamosi.

Katika zaidi ya miji 12, polisi waliwaweka kizuizini watu 401 ilipofika Jumamosi usiku, kwa mujibu wa kundi la haki za binadamu la OVD-Info ambalo linafuatilia wanaokamatwa kisiasa na kutoa msaada wa kisheria.

Forum

XS
SM
MD
LG