Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:17

Wakazi wa Damascus watoa wito wa umoja



Watu wamekusanyika kufuatia mlipuko katika gari
Watu wamekusanyika kufuatia mlipuko katika gari

Maafisa 14 wa polisi waliuwawa katika shambulizi la kushtukiza lililofanywa na wapiganaji watiifu kwa serikali iliyopinduliwa katika mji wa Tartous utawala wa mpito umesema.

Huku maandamano na amri ya kutotoka nje kwingineko ni matukio yanayoashiria kuenea kwa ghasia tangu utawala wa Bashar al-Asaad kupinduliwa wiki mbili zilizopita.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Syria ameandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Telegram kwamba polisi 10 pia walijeruhiwa na kile alichokiita “mabaki” ya serikali ya Assad huko Tartous.

Polisi wa Syria pia waliweka amri ya kutotoka nje katika mji wa Homs, vyombo vya habari vimeripoti baada ya ghasia huko kuhusisha maandamano ambayo wakazi wanasema yaliongozwa na waumini wa waislamu wa adhehebu ya walio wachache ya Alawite na Shia.

Hata hivyo shirika la habari la Reuters halijathibitisha madai ya waandamanaji au kiwango cha vurugu zilizojitokeza.

Forum

XS
SM
MD
LG