Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:32

Mazungumzo ya amani ya Yemen yachelewa kuanza


Wavulana wananchungulia kwenye shimo ambalo limetobolewa na shambulizi la anga lililofanywa na Saudi Arabi kwenye daraja huko Sanaa, Yemen.
Wavulana wananchungulia kwenye shimo ambalo limetobolewa na shambulizi la anga lililofanywa na Saudi Arabi kwenye daraja huko Sanaa, Yemen.

Wajumbe wa Yemen kutoka pande zinazo zozana walitarajiwa kuanza mazungumzo ya Amani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa mapema leo nchini Kuwait, lakini yanaonekana kucheleweshwa kutokana na waasi kushindwa kuwasili.

Serikali ya Yemen inawalaumu waasi wa kihouthi kwa kuchelewesha shughuli hiyo kwa maksudi inayolenga kumaliza mzozo wa miezi 18 ambapo zaidi ya watu 6,000 wameuwawa na kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Msemaji wa kundi la wahouthi Mohammed Abdul Salam amegusia suala la maridhiano kupitia vyombo vya habari vya Kuwait akiomba kuwe na mamlaka itakayosimamia awamu ya mpito ili kutatua kila mzozo wa kisiasa.

Umoja wa Mataifa ulifadhili awamu mbili za mazungumzo mwaka uliopita ingawa hayakufaulu.

XS
SM
MD
LG