Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 20:38

Wajumbe wa ulaya waondoka kwenye sherehe ya Rais Museveni


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akipokea ngao kama ishara ya kukabidhiwa madaraka.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akipokea ngao kama ishara ya kukabidhiwa madaraka.

Wajumbe wa Marekani, Canada na ulaya walitoka kwenye sherehe za kuapishwa Rais wa Uganda zilizofanyika Alhamis katika kujibu kuwepo mshukiwa wa shutuma za uhalifu wa vita na matamshi ya Rais Yoweri Museveni kuikosoa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kwamba ujumbe wa Marekani uliondoka kwenye sherehe za mjini Kampala, ambazo zilihudhuriwa na Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, ambaye amefunguliwa mashtaka na mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko mjini The hague kwa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu katika mkoa wa Darfur uliokumbwa na vita nchini Sudan.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Elizabeth Trudeau alisema Marekani ina wasi wasi kwamba Rais Bashir aliweza kusafiri kwenda Uganda. Uganda ni mwanachama wa ICC na ilitakiwa kumkamata na kumkabidhi kwenye mahakama hiyo mshukiwa yeyote aliyepo kwenye ardhi yake. Lakini katika hotuba yake ya kula kiapo, Museveni alizungumza wazi kutoiheshimu mahakama hiyo.

XS
SM
MD
LG