Wanajeshi waloasi wametangaza amri ya kutotoka nje Alhamisi baada ya kushambulia Ikulu ya rais usiku wa Jumatano
Wanajeshi hao walianza uwasi siku ya Jumatano kwa kupambana na wanajeshi watifu na serikali, na kuchukua udhibiti wa uwanja wa ndege, bunge, na kituo cha taifa cha redio na televisheni.
Waasi wanadai kwamba serikali haijawapa silaha zinazohitajika kukabiliana na uwasi unaofanywa wa watu wa kabila la Tuareg kaskazini mwa nchi.
Msemaji wa waasi aliyejitambulisha kama Luteni Amadou Konare alisema "Kamati ya Kujenga upya Demokrasia na Kudumisha hadhi ya Taifa, imefikisha ukingoni "utawala wa kizembe" wa rais Amadou Toumani Toure.
Luteni Konare alilani serikali ya Toure kutoweza kupambana na ugaidi na kusema wanajeshi watapanga njia za kurudisha utawala kwa raia.
Rais Toure hajasema lolote kutokana na tangazo hilo.