Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 06:27

Polisi Ujerumani yawadhibiti waliopanga kuhujumu marathon


Maafisa wa polisi wakilinda doria katika mbio za nusu -marathon mbele ya Kanisa la Berlin, Berlin, Ujerumani, April 8, 2018.

Vyombo vya usalama nchini Ujerumani vimewakamata watu sita Jumapili wakidaiwa kujihusisha na mpango wa kufanya shambulizi linalofungamana na siasa kali wakati wa michezo ya Berlin ya nusu-marathon.

Katika tamko la pamoja, waendesha mashtaka na polisi wamesema, “Kulikuwa na ishara zilizojificha kuwa wale waliokamatwa, umri kati ya miaka 18 na 21, walikuwa wanashiriki katika maandalizi ya kutenda jinai hiyo wakati wa michezo hiyo.”

Gazeti la German daily Die Welt mara ya kwanza liliripoti kuwa polisi walikuwa wamefanikiwa kuzuia mpango wa shambulizi lililokuwa likiwalenga watizamaji wa mbio hizo na washiriki wa michezo hiyo kwa kutumia visu.

Gazeti hilo pia limeripoti washukiwa wakuu hao kwa namna fulani walikuwa wanafahamiana na Anis Amri, mkimbizi mwenye asili ya Tunisia ambaye aliuwa watu 12 alipoteka lori moja na kuparamia kundi kubwa la watu waliokuwa katika soko la Krismas huko Berlin Disemba 2016.

Kukamatwa kwa watu hao kumekuja baada ya jeshi maalum la polisi la Ujerumani kuendesha msako katika nyumba za washukiwa wa kikundi cha mrengo wa kulia cha Berlin, wakipekua iwapo kuna silaha, Ofisi ya serikali kuu ya mwendesha mashtaka Ujerumani imesema.

Vyombo vya usalama hata hivyo havikueleza iwapo matukio hayo mawili yanamafungamano.

XS
SM
MD
LG