Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:25

Netanyahu na Abbass wakubali kukutana tena Mashariki ya Kati.


Bi.Clinton, mjumbe Mitchell, rais Abbass na waziri mkuu Benyamin Netanyahu wakifanya mazungumzo ya amani, mjini Washington.
Bi.Clinton, mjumbe Mitchell, rais Abbass na waziri mkuu Benyamin Netanyahu wakifanya mazungumzo ya amani, mjini Washington.

Bi. Clinton awapongeza viongozi wa Israel na Palestina kwa kukubali kuendelea na mazungumzo ya amani.

Kwenye sherehe katika chumba cha Benjamn Franklin cha wizara ya mambo ya nchi za nje, waziri Clinton alisema utawala wa Obama umedhamiria kusonga mbele katika kupatikana makubaliano ya amani katika kipindi cha mwaka ujao.

Alisisitiza kuwa kazi kuu itabidi kufanywa na waziri mkuu wa Israel Benjamni Netanyahu na rais wa Palestine Mahmoud Abbass.

“Tunaamini kuwa waziri mkuu na rais mnaweza kufaulu na tunafahamu kuwa mnavyo fanya jambo hili ni kwa maslahi ya usalama wa taifa la Marekani pia. Lakini hatuwezi na hatuta lazimisha suluhisho lolote,” alisema Bi.Clinton.

Bi. Clinton aliketi baina ya Bw. Netanyahu na Bw. Abbass, kwenye meza ilokuwa na taa zakung'ara ziloninginia . Aliwapongeza viongozi hao kwa kukubali kurudia kwenye majadiliano. Lakini alionya kuwa, siku ngumu zinakuja katika juhudi za kubuni taifa huru la kipalestina na usalama kwa Israel.

“Bila shaka kutakuwa na vizuizi na kushindika kwa mambo. Wale wanopinga njia ya amani watajaribu kila njia ya kuhujumu utaratibu huu kama tulivyoshuhudia wiki hii,” alisema Bi. Clinton.

Ghasia daima zimetishia kuharibu juhudi za amani.

Katika siku za karibuni mashambulizi yaliwauwa walowezi wanne wa kiyahudi huko ukanda wa Magharibi. Kundi la wanamgambo la kipalestina la Hamas, ambalo linatawala ukanda wa Gaza na amablo linapinga mazungumzo ya amani na Israel lilidai kuwajibika na mashambulizi hayo.

Waziri mkuu Netanyahu alisema mashambulizi kama hayo yanatishia majadiliano na yanamulika haja ya Israel ya kua na usalama.

“Wanataka kuuwa watu wetu, kuuwa taifa letu kuuwa amani yetu , na kwahiyo ni lazima tupate usalama. Usalama ndio msingi wa amani,” alisema Bw. Netanyahu.

Mtihani wa kwanza wa mazungumzo ya amani utakuja baadae mwezi huu. Mda wa kuzuia kwa miezi 10, ujenzi wa makazi ya walowezi huko ukanda wa Magharibi na Jerusalem Mashariki unamalizika tarehe 26 mwezi huu.

Bw. Abbass amesema majadiliano yatasitishwa ikiwa Israel haitongeza muda wa kusitisha ujenzi wa makazi ya walowezi.

Majadiliano ya moja kwa moja ni ya kwanza kufanyika tangu juhudi za mwisho kuvunjika hapo December mwaka 2008. Utawala wa Obama umetumia miezi 20 yake ya kwanza madarakani kuzirai pande hizo mbili kurejea kwenye meza ya mazungumzo. Hata hivyo, licha ya kuanzishwa mazungumzo, mwanya baina ya pande hizo mbili ni mkubwa na kuna hali ya kuto kuaminiana baada ya miaka ya ghasia na mivutano. Wapalestina wanataka kubuni taifa lao kwenye maeneo ambayo Israel iliteka katika vita vya Mashariki ya kati hapo mwaka 1967, na pia inataka Jerusalem Mashariki kuwa mji wao mkuu. Bw. Netanyahu anakubaliana na wazo la kuwepo na taifa la Kipalestina, lakini anataka kuwepo kwa masharti muhimu bila kuhusisha Jerusalem Mashariki.



XS
SM
MD
LG