Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:13

Waislamu Kenya walalamika kunyanyaswa vijana wao.


Viongozi wa jumuia ya kislamu huko Nairobi walitoa taarifa siku ya Alhamisi kulaani hatua yan polisi kuwasaka na kuwanyanyasa vijana wa kislamu kwa madai ya kuhusika na vitendo vya ugadi.

Viongozi hao wanadai vijana wa kislamu wanaishi kwa uwoga wa kuvamiwa na kutiwa nguvuni na polisi na hatimae kuwekwa kizuizini au hatimae kusafirishwa katika nchi za nje kwa mashtaka ya ugaidi.

Mapema wiki hii katika mitaa ya Pumwani, Eastleigh na Kawangare, huko mjini Nairobi, vijana wa kiislamu walivamiwa usiku na kutiwa mbaroni kwa madai ya kuhusika na ugaidi.

Kikosi maalum cha kupambana na ugaidi nchini Kenya, walivamia mtaa wa Pumwani usiku wa Jumatano, na kuwakamata vijana kadhaa wa kiislam. Viongozi wa kiislam mjini Nairobi, wamesema ni makosa kwa vijana wa kiislamu kukamatwa kiholela na kinyume na sheria. Mwenyekiti wa chama taifa cha waislamu, Abdillahi Abdi, alisema hawawezi kukubaliana na visa vya kigaidi vinavyotekelezwa na mkenya yeyote yule nchini humo au mahala kwengine. Anasema sheria ya kusafirisha magaidi bila makosa yeyote, inapasa kuwahusisha wakenya wote bila ubaguzi.

Msemaji wa polisi, Eric Kiraithe alisema polisi nchini Kenya hawakuvunja sheria yeyote, lakini walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kulinda usalama wa raia.

XS
SM
MD
LG