Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 11:44

Waislam duniani wameanza mwezi mtukufu wa Ramadan


Baadhi ya waislam huko Afrika wakisoma kuran kwenye mfungo wa Ramadan

Nchini Marekani inakadiriwa waislamu milioni 3.2 watafunga mnamo mwezi huu wa Ramadani ikiwa ni karibu asilimia 10 ya wakazi milioni 327 wa Marekani

Mwezi mtukufu wa Ramadan umeanza Jumatatu kwa waislam wapatao bilioni moja, milioni mia sita duniani ambapo inawabidi kutekeleza ibada na kufunga kuanzia alfajiri hadi magharibi na baada ya hapo hujumuika pamoja kwa chakula cha jioni "Iftar".

Ramadan huanza mwezi wa tisa wa kalenda ya ki-Islam ambapo waislam wanaamini kuran takatifu iliwasilishwa kwa Mtume Mohammad katika karne ya saba. Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadan waislamu wanatarajiwa kuwa wakarimu kwa kuwasiadia watu wasiojiweza na ndani ya mwezi huu mtukufu kuna siku 10 za mwisho za kukamilisha mfungo ambazo zinachukuliwa kuwa siku takatifu zaidi ambazo watu hulala kwenye misitiki wakitafuta neema zaidi ya mwenyezi mungu katika masiku yanayotoa siku maalumu iitwayo "Lailatul Kadri" usiku mtukufu wa mwaka kwa kalenda ya ki-Islam.

Nchini Marekani inakadiriwa waislamu milioni 3.2 watafunga mnamo mwezi huu wa Ramadani ikiwa ni karibu asilimia 10 ya wakazi milioni 327 wa Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG