Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 19:54

Wahariri wawili wakamatwa Zambia


Gazeti la 'The Post,' nchini Zamboa
Gazeti la 'The Post,' nchini Zamboa

Polisi nchini Zambia wamewakamata wahariri wawili wa vyeo vya juu wa gazeti la 'The Post' la nchini humo.

Waliowekwa kizuizini ni Fred Mmembe, mhariri mkuu wa The Post, mke wake Mutinta, pamoja na mhariri msaidizi Joseph Mwenda.

Walishikiliwa kwa usiku mmoja na wanasema walipigwa na kushtakiwa kwa uhalifu wa mali na kutoa hati za uongo.

Hati iliyoamriwa ilitolewa na mahakama ya rufaa ya kodi ikielezea kufungwa kwa gazeti hilo kutokana na kutolipa kodi.

Wahariri hao wanasema tukio hilo lilitokea wakati wakipokea nakala ambazo zinawataka kurudi kwenye ofisi zao. Wahariri hao kisha walichukua amri ya mahakama kwenda kituo cha polisi ambao walikuwa wakilinda ofisi za gazeti hilo.

"Kwa wakati fulani uamuzi ulitolewa kwamba hatutakiwi kupata fursa ya kurudi," alisema Mwenda.

XS
SM
MD
LG