Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 18, 2026 Local time: 12:08

Wahanga wa mafuriko Kinshasa wafikia 44

Mtaa wa katikati wa Kinshasa umefunikwa kwa maji  Alhamisi Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
1/8 Mtaa wa katikati wa Kinshasa umefunikwa kwa maji  Alhamisi Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Garilililozama katika mafuriko ya Kinshasa,Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
2/8 Garilililozama katika mafuriko ya Kinshasa,Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Mafuriko makubwa katika mji wa Kinshasa, yazamisha magari Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
3/8 Mafuriko makubwa katika mji wa Kinshasa, yazamisha magari Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Mafuriko katika kitongoji mashuhuri cha Limete mjini Kinshasa, Januari 4 2017. (VOA/TopCongo)
4/8 Mafuriko katika kitongoji mashuhuri cha Limete mjini Kinshasa, Januari 4 2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Mitambo ya umeme imefunikwa na maji yanayotokana na mvua nyingi ya siku moja mjini Kinshasa Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
5/8 Mitambo ya umeme imefunikwa na maji yanayotokana na mvua nyingi ya siku moja mjini Kinshasa Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Mafuriko kwenye kituo cha umeme cha kampuni ya taifa ya umeme mjini Kinshasa Januari 4 2017. (VOA/TopCongo)
6/8 Mafuriko kwenye kituo cha umeme cha kampuni ya taifa ya umeme mjini Kinshasa Januari 4 2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Mfanyakazi wa kampuni ya taifa ya umeme (SNEL) akisimama ndani ya maji ya mafuriko kwenye uwanja wa kituo cha umeme Kinshasa, Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
7/8 Mfanyakazi wa kampuni ya taifa ya umeme (SNEL) akisimama ndani ya maji ya mafuriko kwenye uwanja wa kituo cha umeme Kinshasa, Januari 4, 2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Jiji la Kinshasa limefurika kwa maji kutokana na mvua ya usiku moja  2017. (VOA/TopCongo)
8/8 Jiji la Kinshasa limefurika kwa maji kutokana na mvua ya usiku moja  2017. (VOA/TopCongo)
Onyesha zaidi Show less
Previous slide
Next slide

Mafuriko na maporomoko yameuwawatu 44 katika vitongoji kadhaa vya mji mkuu Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jiji la tatu kwa ukubwa Afrika, afisa mmoja amesema Ijumaa.

“Tuna idadi ya vifo ya mwisho ambayo inaonyesha watu 44 wamekufa,” amesema waziri wa afya na masuala ya jamii wa jimbo hilo, Dominique Weloli. Idadi ya awali ya waliopoteza maisha ilikuwa ni watu 37.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP robo tatu ya makazi ya wananchi wa Kinshasa ni vibanda ambavyo havina mfumo maji taka wala umeme, kwa mujibu wa aliyekuwa mkuu wa shirika la UN-Habitat, Corneille Kanene.

Mvua kubwa na maporomoko yaliyotokea usiku kucha Jumatano yaliharibu nyumba hizo ambazo zilikuwa zimejengwa pembeni ya mlima.

Kinshasa ambayo ni makazi ya watu takriban milioni 10, ni jiji la tatu lenye watu wengi Afrika baada ya Cairo na Lagos.

This item is part of
XS
SM
MD
LG