Meli kubwa ya mizigo iliangusha daraja hilo Jumanne baada ya kugonga mojawapo ya nguzo zake kuu. Wataalam wanajaribu kufikiria jinsi ya “kukata daraja hilo katika vipande sawa vya ukubwa ambavyo tunaweza kuinua,” Kamanda mkuu wa kikosi cha walinzi wa pwani Admirali Shannon Gilreath alisema Ijumaa katika mkutano na wanahabari. Zana zinazohitajika zimeanza kutumika.
Ni pamoja na Kreni saba za kuinua mizigo, za kuelea majini, mojawapo ikiwa ni kubwa zaidi kwa kanda nzima ya mashariki mwa Marekani, yenye uwezo wa kuinua tani 1,000, boti 10 za kuvuta, mashua tisa, boti nane za kubeba mizigo, na boti tano za Walinzi wa Pwani.
Forum