Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:31

Wahamiaji wawili wafariki nchini Morocco baada ya boti lao kuzama.


Mwili wa kijana mmoja ukifunikwa na blanketi baada ya kuokotwa na polisi wa Uispania kwenye maji karibu na mpaka kati ya Morocco na Uispania, Mei 20, 2021. Picha ya AP.
Mwili wa kijana mmoja ukifunikwa na blanketi baada ya kuokotwa na polisi wa Uispania kwenye maji karibu na mpaka kati ya Morocco na Uispania, Mei 20, 2021. Picha ya AP.

Wahamiaji wawili wamekufa maji baada ya boti lao kuzama na zaidi ya 200 wengine waliwekwa kizuizini wakati wakijianda kuondoka Morocco kwa njia ya bahari, shirika la habari la serikali MAP limeripoti Jumapili.

Miili ya wahamiaji hao wawili ilionekana juu ya majii baada ya boti lao kuzama, MAP imeripoti bila kutoa maelezo zaidi.

Katika tukio jingine, maafisa wa Morocco waliwakamata wahamiaji 236 katika operesheni za msako Ijumaa na Jumamosi katika mkoa wa kusini wa Tarfaya na mji wa Laayoune, mji mkuu wa eneo lenye ugomvi la Western Sahara.

Inaarifiwa kuwa wahamiaji hao walikuwa wanataka kuvuka kuelekea visiwa vya Spain vya Canary.

Mkoa wa Tarfaya unapatikana umbali wa kilomita 100 na visiwa vya Canary na kimekua kituo kikuu cha usafiri kwa wahamiaji wanaotarajia kufika Ulaya.

XS
SM
MD
LG