Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:45

Wahamiaji kadhaa kutoka Afrika wazuiliwa Saudi Arabia katika mazingira mabaya


Saudi Arabia inawazuilia mamia ya wahamiaji, wengi wao kutoka Ethiopia katika mazinira mabaya sana mjini Riyadh.

Kulingana na shirika la kufuatilia haki za kibinadamu, baadhi ya wahamiaji hao wameteswa au kupigwa.

Wahamiaji wanaozuiliwa, wengi wao kutoka Ethiopia na baadhi kutoka nchi zingine za Afrika na Asia, wanasubiri kurudishwa katika nchi zao.

Walikamatwa na maafisa wa Saudi Arabia kwa sababu hawana vibali vya kuishi nchini humo.

Ripoti iliyotolewa jumanne, inawanukuu wahamiaji hao wakisema kwamba wanazuiliwa katika mazingira mabaya sana yenye idadi kubwa ya watu na kwamba wamepigwa na walinzi wanaotumia vyuma vilivyowekwa mpira juu yake.

Kuna madai kwamba wahamiaji watatu wamekufa kutokana na mateso hayo.

Shirika la human rights watch limesema kwamba limezungumza na raia wa Ethiopia saba na raia wa India wawili, mnamo mwezi uliopita wakiwa kizuizini wakisubiri kurudishwa makwao.

Wawili kati ya waliohojiwa wamesema kwamba wamekuwa wakizuiliwa kwa zaidi yam waka mmoja na hakuna hatua zinazhukuliwa kuwakinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona licha ya kwamba baadhi yao wameonyesha dalili za kuambukizwa virusi hivyo.

Maafisa wa Saudi Arabia hawajasema lolote kuhusu ripoti hiyo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG