Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:14

Wahamiaji 29 waokolewa baharini wakielekea Italy


Wahamiaji wakiwa katika boti kuelekea Italy
Wahamiaji wakiwa katika boti kuelekea Italy

Walinzi wa pwani wa Ugiriki wamewaokoa wahamiaji 29 kutoka kwenye boti chakavu kwenye kisiwa cha magharibi cha Lefkada walipokuwa wakielekea Italy.

Mamlaka zinasema uokozi wa Jumapili ni wa kwanza uliohusisha wahamiaji waliokuwa wakijaribu kuvuka kutoka Ugiriki kwenda Italy tangu Athens ifunge mpaka wake wa ardhini kuelekea kwingine ulaya hapo mwezi Machi.

Watoto wawili wameripotiwa kuwemo kwenye boti ndogo ambayo iligundulika ikielea karibu na Lefkada.

Ripoti za ndani zimesema nahodha ambaye aliiacha boti hiyo alikuwa sehemu ya harakati za usafirishaji binadamu kwa njia ya magendo. Haijulikani mahali alipo nahodha huyo.

Wahamiaji wakiwa katika boti za uokozi huko Sicily, Italy. Mei 6, 2016. Italy's coast guard has rescued about 1,000 people off the c
Wahamiaji wakiwa katika boti za uokozi huko Sicily, Italy. Mei 6, 2016. Italy's coast guard has rescued about 1,000 people off the c

Kabla ya kufunga mpaka wake na Macedonia mwezi Machi maelfu ya wahamiaji walisafiri upande wa kaskazini kupitia Ugiriki wakielekea kwenye usalama na mafanikio nchini Ujerumani na kulenga maeneo mengine ya ulaya magharibi.

Kufunguwa huko kwa mpaka kumesababisha maelfu ya wahamiaji kukwama nchini Ugiriki wengi wao wakikabiliwa na vitisho vya kurejeshwa nchini Uturuki kama sehemu ya msukumo wa ulaya kuzuia mmiminiko wa wakimbizi kutoka nchi zilizokumbwa na vita za Syria na Iraq.

XS
SM
MD
LG