Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:50

Clinton na Sanders wazidi kuchuana


Kampeni kati ya wagombea urais kwa chama cha Democrat hapa Marekani, Hillari Clinton na Bernie Sanders, zimeendelea kutia fora wakati wakibadilishana maneno ya ni nani anefaa zaidi kuwa rais.

Hillary Clinton Jumatano alimshambulia Sanders ambae ni seneta wa Vermont kutokana na matamshi yake mahojiano na gazeti la New York Times ambapo alishindwa kuelezea atakavyofanya ili kuvunja makampuni makubwa ya kifedha hapa Marekani. Akihutubia wafuasi wake katika jimbo la Philadelphia, Clinton alisema mgombea anafaa kutekeleza mambo na wala sio kutupa mikono hewani pekee anapoeleza agenda zake.

Naye Sanders baadae katika jimbo hilo hilo alisema kuwa Clinton hafai kuwa rais wa Marekani kutokana na mambo mengi alioyaidhinisha akiwa seneta likiwa swala na vita vya Iraq vya 2003.

XS
SM
MD
LG