Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 18:20

Wagombea urais wa Republican wapambana


Mgombea wa Republikan na Gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney akizungumza kwenye mkutano wa kampeni huko Canton, Ohio.

Gavana wa zamani Mitt Ropmney kuchuana vikali na Santorum kwenye majimbo 10 Jumanne.

Wagombea kiti cha rais kutoka chama cha Republican hapa Marekani wamo katika harakati nyingi kabla ya chaguzi za awali Jumanne inayofahamika Marekani kama “Super Tuesday” ambapo chaguzi hizo zitafanyika katika majimbo 10. Gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney yupo kwenye ushindani mkali na Rick Santorum seneta wa zamani wa Marekani katika kinyang’iro kinachofuatiliwa kwa karibu sana hasa katika jimbo la Ohio. Kura mpya ya maoni inaonyesha wanasiasa hao wawili wakiwa sawa huko Ohio. Kura ya maoni ya Quinnipac inaonyesha kuwa Romney amepata nguvu mpya tangu wiki iliyopita na sasa ana asilimia 34 ya wapiga kura wa Republican, akiwa na pointi 3 tu mbele ya Santorum. Mwishoni mwa February Santorum aliongoza huko Ohio.

XS
SM
MD
LG