Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:58

Wagombea urais Marekani wafanya kampeni tofauti katika jimbo moja


Siku chache kabla ya mkutano mkuu wa vyama kuwaidhinisha rasmi wagombea urais Marekani.
Siku chache kabla ya mkutano mkuu wa vyama kuwaidhinisha rasmi wagombea urais Marekani.

Kampeni za kuwania urais nchini Marekani zinaelekea kusini mwa nchi kwenye jimbo la North Carolina siku ya Jumanne ambapo wote m-Republican Donald Trump na m-Democrat Hillary Clinton wanafanya mikutano huko.

Trump atakuwa na mkutano jioni ya Jumanne huko Raleigh mji mkuu wa jimbo hilo. Saa chache kabla ya hapo Clinton atakuwa umbali wa kilomita 200 huko Charlotte huku Rais Barack Obama akionekana kwa mara ya kwanza katika kumuunga mkono mwanamke ambaye alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani wakati wa muhula wake wa kwanza madarakani.

Wakitarajia kufanya kampeni za kisiasa pamoja Clinton aliandika kwenye mtandao akiambatanisha video ya rais iliyorekodiwa mwezi uliopita akimuunga mkono mgombea huyo.

Miaka minane iliyopita, Obama na Clinton walishindana katika uchaguzi wa awali uliokuwa na mvutano ambao uliishia kwa Obama kupata uteuzi wa chama cha Democrat na Clinton alimfanyia kampeni katika uchaguzi mkuu dhidi ya m-Republican John McCain.

XS
SM
MD
LG