Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 21:23

Marais wa zamani na wa sasa waonyesha nia ya kugombea urais Ivory coast


Aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Henri Konan Bedie

Tume ya uchaguzi nchini Ivory Coast imeahidi kuandaa uchaguzi huru na haki  huku chama kinachotawala cha RHDP kikimtaka rais Alassane Ouattara kugombea mhula mwingine madarakani wakati wa uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

Wapinzani hata hivyo wanasisistiza kwamba Outtara hana haki ya kikatiba kugombea mhula wa tatu madarakani.

Hatua hiyo inaonekana kuwa mtihani mkubwa kwa hali ya amani na utulivu ambayo imerejea Ivory Coast, tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua watu 3,000 kati ya mwaka 2010 na 2011.

Ushindi wa Ouattara, uliokumbwa na utata mwaka 2010, ulisababisha ghasia na umwagikaji wa damu, vyama vya upinzani vikidai kwamba tume ya uchaguzi ilimpendelea Ouattara.

Tume ya uchaguzi inasema inapanga kufanya mabadiliko makubwa katika utendakazi wake, na kushirikisha vyama vyote vya kisiasa katika uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa tume hiyo Ibrahime Coulibaly Kuibert, amesema kwamba “lengo letu la msingi ni kuhakikisha kwamba uchaguzi unaandaliwa kwa njia huru na haki”.

Ouattara ameomba mda zaidi kufikiria iwapo atakubali ombi la chama chake kugombea tena urais, akisema kwamba “Sijawahi kukosa kuwaridhisha”.

Amesema kwamba atatangaza uamuzi wake kupitia kwa hotuba kwa taifa Agosti 6.

Wapinzani wake Ouattara wanasema kwamba katiba inamzuia kugombea urais kwa mhula mwingine tena, lakini Ouattara anasema mihula yake miwili ya kwanza haiwezi kuhesabiwa kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2016.

Wagombea wengine wa urais ambao wametangaza rasmi nia yao ni aliyekuwa rais wa nchi hiyo kati yam waka 1993 na 1999 Henri Konan Bedie, na ambaye ni kiongozi wa mojawapo ya vyama vikuu vya upinzani nchini Ivory Coast - PDCI.

Aliyekuwa rais wa nchi hiyo ambaye alikuwa amekatalia madarakani licha ya kushindwa la Ouattara, na ambaye alifutiwa mashitaka ya uhalifu wa kibinadamu dhidi yake katika mahakama ya ICC Laurent Gbagbo, hajatangaza rasmi iwapo atagombea tena urais kupitia chama chake cha FPI japo ameasilisha maombi ya kutaka kupewa pasipoti ili arejee nchini mwake, hatua inayotajwa kama ya kijitaarisha kugombea urais.

-Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG