Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 06, 2021 Local time: 00:58

Wafungwa wawili wa Gereza la Guantanamo wamehamishiwa Ghana


Wafungwa wawili wa Gereza la Guantanamo Bay, Cuba

Wafungwa wawili kutoka gereza la Guantanamo Bay, Cuba wamehamishiwa nchini Ghana kwa makazi mapya wizara ya ulinzi ya Marekani imeeleza jana jumatano.

Watu hao wawili raia wa Yemen Mohamed Omar Mohamed BIN Atef na Khalid Mohamed Salih al Dhuby walikuwa wakishikiliwa kama maadui wa kivita bila kufunguliwa mashitaka kwa karibu miaka 14.

Guantanamo, Cuba
Guantanamo, Cuba

​Kufuatia uchambuzi wa kina kwa kesi zao, imeamuliwa kwamba washukiwa hao wawili si tishio la usalama, maafisa wa Pentagon wameeleza.

“Marelkani inaishukuru serikali ya Ghana kwa juhudi zake za kibinadamu na nia yake ya kuunga mkon o juhudi za kufunga gereza la Guantanamo" alisema msemaji wa Pentagon Garry Ross.

Wakiwa nchini Ghana watakuwa chini ya uangalizi mkali wa maafisa aliongeza.

XS
SM
MD
LG