Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:40

Wafungwa 34 watoroka gerezani DRC


Moja ya magereza ya Congo.
Moja ya magereza ya Congo.

Afisa mmoja nchini DRC anasema wafungwa 34 wametoroka gerezani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC baada ya kuuvunja ukuta wakati wa mvua mkubwa iliyokuwa inanyesha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Asociated Press-AP waziri wa sheria wa jimbo la kivu kusini Pasaline Basezage alisema Jumatatu kwamba takriban wafungwa 27 waliotoroka Jumapili jioni walikuwa wamekutwa na hatia kwa makosa ya uhalifu wa ngono na vitendo vingine vya ghasia.

Gereza la Mwenga lililopo kiasi cha kilometa 130 kusini ambalo lilikuwa linawashikilia wafungwa 42 wakati huo. Afisa wa gereza la Mwenga, Desire Masumbuko alisema majeshi ya usalama yamewakamata wafungwa wanne waliotoroka.

Baadhi ya wakazi huko mashariki mwa Congo
Baadhi ya wakazi huko mashariki mwa Congo

Afisa Masumbuko aliwataka wakazi kuwa katika hali ya tahadhari na kushirikiana katika kuwasaka wafungwa waliobaki. Maelfu ya wafungwa wameshawahi kufanikiwa kutoroka gerezani kote nchini Congo tangu mwezi Mei wakati wanachama wa dhehebu moja la kikristo walipovamia gereza moja mjini Kinshasa. Walioshuhudia wanasema maelfu ya wafungwa walitoroka.

XS
SM
MD
LG