Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 17:30

Wafuasi wa uhuru wa kujieleza Nigeria wapata wasiwasi


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Wakili wa Yahaya Aminu Sharif alidai kesi yake inapaswa kusikilizwa katika mahakama ya kawaida ili kupinga uhalali wa mahakama za kiislamu Nigeria ambazo wakosoaji wanasema zinatishia uhuru wa kujieleza.

Katika uamuzi uliotolewa kwa njia ya mtandao wa Zoom , mahakama ya rufaa ya Kano ilisema katika uamuzi wake kwamba sheria ya Shari au ya kiislamu haikiuki katiba ya kitaifa na kwamba mahakama za kiislamu zina mamlaka ya kusikiliza kesi za matukio ya kukufuru.

Uamuzi huo ulitupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na wakili wa mwimbaji Yahaya Aminu Sharif , Kola Alapini akihoji uhalali wa hukumu ya kifo.

Mmoja wa majaji Abubakar Muazu Lamido alisema changamoto haiungwi mkono na sheria na kwamba ni zaidi ya hisia.

Mahakama ya Kiislamu mjini Kano ilimuhukumu kifo Sharif August mwaka 2020 kwa madai ya kusambaza wimbo uliomkashifu mtume Mohamed katika mitandao ya kijamii, ambapo mwezi Novemba mahakama kuu ilibadilisha hukumu hiyo na kuamuru kusikilizwa upya katika mahakama ya sharia ikisema kwamba Sharif hakuwa na uwakilishi wowote wa kisheria wakati wa kesi yake.

Wanaharakati wanazua wasiwasi kuhusu uamuzi wa mahakama ya rufaa. Wakili wa haki za binadamu anayeishi Abuja Martin Obono anasema ni tishio kwa uhuru wa kujieleza.

XS
SM
MD
LG