Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:19

Wafuasi wa Rais wa zamani wa Brazil wavamia Bunge, Mahakama ya juu na Ikulu


Wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, wakabiliana na polisi katika maandamano nje ya Ikulu, mjini Brazili, Januari 8,2023. Picha ya Reuters
Wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, wakabiliana na polisi katika maandamano nje ya Ikulu, mjini Brazili, Januari 8,2023. Picha ya Reuters

Wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro ambaye alikataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi wa rais, Jumapili walivamia Bunge, Mahakama ya juu na Ikulu katika mji mkuu wa Brazil, wiki moja baada ya kuapishwa kwa mpinzani wake wa mrengo wa kushoto, Rais Luiz Inacio Lula da Silva.

Maelfu ya waandamanaji waliruka vizuizi vya usalama, wakapanda juu ya mapaa, wakavunja madirisha na kuvamia majengo yote matatu, ambayo yameunganishwa na eneo kubwa la Three Powers Square mjini Brasilia.

Wengine waliomba uingiliaji kati wa jeshi ili kumrejesha madarakani Bolsonaro wa mrengo mkali wa kulia na kumuondoa Lula katika urais.

Kituo cha televisheni cha Globo News kilionyesha waandamanaji wakizurura ndani ya ikulu, wengi wao wakiwa wamevalia rangi za kijani na manjano za bendera ya taifa ambazo pia zimeashiria vuguvugu la kihafidhina la taifa hilo lililoanzishwa na Bolsonaro.

Rais huyo wa zamani ambaye alisafiri kuja Marekani kabla ya kuapishwa kwa Lula, alikuwa hajasema chochote kuhusu matukio ya Jumapili.

Matukio hayo yalikumbusha shambulio la Januari 6, 2021 kwenye Bunge la Marekani lililofanywa na wafuasi wa rais wa wakati huo Donald Trump.

XS
SM
MD
LG