Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 14:27

Wafuasi wa magenge wauwawa Haiti


Polisi na makundi ya kiraia ya kujilinda yamewauwa watu 28 wanaodaiwa kuwa wanachama wa genge katika mji mkuu wa Haiti, Port au Prince katika operesheni ya usiku kucha, serikali imesema Jumanne, wakati ikijaribu kurejesha udhibiti wa mji huo.

Hata hivyo, wanachama wa magenge waliendelea na mashambulizi katika baadhi ya wilaya za mji huo wenye ghasia, baada ya mmoja wa viongozi wao kutoa wito Jumatatu jioni kwa serikali ya mpito kuachia ngazi.

Mpiga picha wa shirika la habari la AFP ameona watu wakichoma miili ya watu wanaodaiwa kuwa ni wa magenge barabarani, huku tairi zikiwa zimerundikana juu yao na kuichoma.

Maafisa walisimamisha lori lililokuwa limebeba wanachama wa genge katika kitongoji cha matajiri cha Petion Ville, saa 2:00 asubuhi Jumanne, msemaji wa Polisi ya Haiti, Lionel Lazarre, ameiambia AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG