Polisi wa Algeria wamesema kwamba watu 43 wamethibitishwa kufariki kutokana na moto unaoendele akuteketeza misitu kwa siku kadhaa kaskazini mwa nchi hiyo.
Zaidi ya matukio ya moto 30 yamezimwa wikendi hii, lakini kuna sehemu ambazo moto huo unaendelea kuwaka, na maafisa wamesema kwamba huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka.
Zaidi ya familia 1000 zimeokolewa kutoka sehemu ambazo zimeathiriwa zaidi ikiwemo katika eneo la El Tarf, karibu na mpaka na Tunisia.
Watu 13 wamekamatwa, wakiadaiwa kushiriki karika kuwasha moto huo.