Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:10

Wafaransa wapiga kura leo


Uchaguzi Ufaransa
Uchaguzi Ufaransa

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa Ufaransa, vikifikisha ukingoni kampeni za uchaguzi wa urais wakati wafaransa wengi wanasema ni uchaguzi wenye uadui na utata mkubwa kuliko chaguzi nyingine zote katika historia ya hivi karibuni.

Wanasema ni uchaguzi ambao utaweza kuamua iwapo nchi hiyo itaendelee na utandawazi uliopo duniani au utafute njia mpya, ya kipekee nje ya Umoja wa Ulaya.

Katika kinyang’anyiro kilichogubikwa na utata wa suala la ajira, uhamiaji na usalama, ambapo maamuzi ya wapiga kura katika raundi hii ya pili na ya mwisho Jumapili yako wazi.

Wakati mgombea wa mrengo wa kati, anayetaka kuendelea na Umoja wa Ulaya ambaye ni waziri wa uchumi wa zamani, Emmanuel Macron anachuana na mzalendo, mwenye kupinga uhamiaji Marine Le Pen.

Kura za maoni zilizoendelea kabla ya uchaguzi zilikuwa zinaonyesha kuwa Macron anaongoza kwa kiwango kikubwa cha asilimia 63 dhidi ya mpinzani wake Pen ambaye ana asilimia 37.

Wagombea wote walizungukwa na waandishi wakati wakielekea kupiga kura katika maeneo tofauti.

Macron alipiga kura katika mji uliopo pwani ya Le Tourguet kaskazini ya Ufaransa akiwa pamoja na mkewe, Brigitte Macron.

Le Pen amepiga kura yake huko Henini-Beaumont, mji mdogo ulioko katika himaya ya chama chake cha National Front party.

Rais anaemaliza muda wake Francois Hollande amepiga kura Jumapili katika eneo la kisiasa analolimiliki huko upande wa kusini magharibi wa Ufaransa.

XS
SM
MD
LG