Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:58

Wafaransa waandamana kupinga mipango ya kurekebisha mfumo wa pensheni


Siku ya nne ya maandamano ya kitaifa dhidi ya mageuzi ya pensheni, huko Paris.Februari 11,2023 REUTERS
Siku ya nne ya maandamano ya kitaifa dhidi ya mageuzi ya pensheni, huko Paris.Februari 11,2023 REUTERS

Polisi walijotokeza mitaani kote nchini   Ufaransa  Jumamosi wakati waandamanaji wakifanya duru ya nne ya maandamano ya kitaifa kupinga mipango ya Rais Emmanuel Macron ya kurekebisha mfumo wa pensheni wa nchi hiyo.

Maelfu ya watu walitarajiwa katika siku hii kuandamana katika miji ya Paris, Nice, Marseille, Toulouse, Nantes na miji mingine kwa matumaini ya kuendeleza shinikizo kwa serikali kurejea.

Maandamano hayo yaliwavutia vijana na wengine waliopinga mapendekezo ya pensheni ambao hawakuweza kuhudhuria siku tatu za awali wakati maandamano yalifanyika katika siku za kazi.

Wakati huu, hata hivyo, mgomo wa wafanyakazi wa reli haukuambatana na maandamano hayo na kuruhusu treni za Paris Metro kufanya kazi siku ya Jumamosi. Hata hivyo, mgomo usiotarajiwa wa wafanyakazi wa kuongoza ndege ulimaanisha kwamba hadi nusu ya safari za ndege kuingia na kutoka katika uwanja wa ndege wa pili kwa ukubwa wa Paris, Orly, ziliahirishsiku ya wa Jumamosi alasiri.

Huko Paris, baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi ambao walitaka kupaza sauti zao za upinzani walihudhuria maandamano hayo kwa mara ya kwanza, kutokana na kazi nyingi za siku za wiki.

XS
SM
MD
LG